• Kuhusu HabariLEO
  • Matangazo: Maelekezo & Bei
  • Nunua E-Paper
HabariLeo
No Result
View All Result
No Result
View All Result
HabariLeo
No Result
View All Result

Makongoro aibuka mshindi safari ya Kombe la Dunia

Na Grace Mkojera by Na Grace Mkojera
May 12, 2026
in Michezo na Burudani
1
Makongoro aibuka mshindi safari ya Kombe la Dunia

DAR ES SALAAM:MAKONGORO Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa Julius Nyerere, ameingia katika orodha ya washindi watatu wa droo ya kampeni ya Kombe la Dunia ya benki ya CRDB hatua ambayo imezua mvuto wa kipekee kutokana na historia ya familia yake nchini.

Makongoro alitangazwa mshindi wa safari ya kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia 2026 itakayofanyika Canada, Marekani na Mexico, na baada ya kupigiwa simu kuthibitishiwa ushindi wake alijibu kwa kifupi: “Asante sana.”

Ushindi wake umeonekana kubeba taswira ya kipekee ya urithi wa familia ya Nyerere, ambapo jina la Baba wa Taifa linaendelea kuhusishwa na matukio makubwa ya kitaifa na kimataifa hata katika nyanja tofauti kama michezo na burudani.

Wengine waliobahatika katika droo hiyo ni mfanyabiashara maarufu Arun Lodhia pamoja na Abdulraouf Suleiman, ambao nao wataungana katika safari hiyo ya kihistoria ya kushuhudia Kombe la Dunia.

Katika upande wa zawadi za vifaa vya elektroniki, washindi wa televisheni ni Arina Kaswala, Lusekelo Michael na Easter Kabakama.

Akizungumza wakati wa droo hiyo iliyofanyika Dar es Salaam, Karington Chahe amesema kampeni hiyo imeendelea kuwapa nafasi wateja wa benki hiyo kushiriki ndoto ya kushuhudia Kombe la Dunia moja kwa moja.

Amesema jumla ya washindi 20 wanatarajiwa kunufaika na kampeni hiyo, ambapo 10 watasafiri kwenda Marekani na Canada, huku wengine wakipata zawadi mbalimbali zikiwemo televisheni za inchi 85 na ving’amuzi.

“Fursa ya Kombe la Dunia ipo kwa Watanzania kupitia matumizi ya TemboCard. Kampeni hii inaendelea na mwezi ujao tutapata washindi wengine watakaokwenda kushuhudia mashindano hayo,” amesema.

Kombe la Dunia 2026 linatarajiwa kufanyika katika nchi tatu za Marekani, Canada na Mexico, likiwa moja ya matukio makubwa zaidi ya michezo duniani.

CRDB Bank imesema kampeni hiyo ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wateja wake pamoja na kuongeza hamasa ya matumizi ya huduma zake za kidijitali.

Previous Post

Kiswaga asaidia mifuko 200 ya Saruji Tosamaganga Sekondari

Next Post

Chevron: Tupo tayari kuwekeza Tanzania

Next Post
Chevron: Tupo tayari kuwekeza Tanzania

Chevron: Tupo tayari kuwekeza Tanzania

Comments 1

  1. ScottMSmith says:
    3 months ago

    I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do….. https://www.work27.info

    Reply

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Zilizosomwa Ziadi

  • Mradi mpya kupunguza msongamano bandari ya Dar
    Mradi mpya kupunguza msongamano bandari ya Dar
  • Kairuki apongeza upanuzi  huduma za intaneti
    Kairuki apongeza upanuzi huduma za intaneti
  • Mbegu bora, chachu ya kilimo cha ushindani
    Mbegu bora, chachu ya kilimo cha ushindani
  • Luizer ampongeza Asha Baraka
    Luizer ampongeza Asha Baraka
  • Luizer awasihi wanawake kutunza ngozi
    Luizer awasihi wanawake kutunza ngozi

Latest on this theme

  • (no title)
    by Yohana Shida, Geita
    September 5, 2022
  • (no title)
    by NEW YORK, Marekani
    September 6, 2022

  • Kuhusu HabariLEO
  • Matangazo: Maelekezo & Bei
  • Nunua E-Paper

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

No Result
View All Result

© 2026 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.