Wizara yaweka lengo Sh bil 1/- mapato 2026/27

DODOMA: WIZARA ya Habari Sanaa na Utamaduni inakusudia kukusanya Sh bilioni 1 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kutoka katika vyanzo mbalimbali.
Vyanzo hivyo ni vitambulisho ya waandishi wa habari, machapisho ya picha, mabango na majarida, usajili wa magazeti, ada ya mwaka ya magazeti, viingilio katika uwanja wa Benjamin Mkapa na Uhuru.
Vyanzo vingine ni ada za upangishaji na matangazo katika eneo changamani la michezo Dar es Salaam pamoja na ada za wanachuo kutoka Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.
Aidha, kwa upande wa taasisi 12 zilizo chini ya wizara hiyo kiasi kinachotarajiwa kukusanywa ni sh bilioni 40.8.



