Kihongosi awasili Mara ziara ya kikazi

MUSOMA: Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, amewasili leo Mei 14, 2026 mkoani Mara Region kwa ajili ya kuanza ziara yake ya kikazi ya siku nne.

Kihongosi amepokewa na viongozi pamoja na wanachama wa CCM ngazi ya Mkoa na Wilaya, ambapo mara baada ya kuwasili alipata nafasi ya kufanya kikao cha ndani na kuzungumza na viongozi wa chama kuhusu masuala mbalimbali ya uhai na uimarishaji wa CCM katika mkoa huo.

Ziara hiyo inalenga kukagua uhai wa chama kupitia mashina, kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM kupitia miradi ya maendeleo pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Aidha, katika ziara hiyo, Kihongosi anatarajiwa kutembelea wilaya za Musoma, Tarime Mjini, Tarime Vijijini, Butiama na Bunda kwa ajili ya kuzungumza na wananchi na viongozi wa chama kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo na uimarishaji wa chama.

Katika ratiba ya leo, Kihongosi anatarajiwa kutembelea mashina mbalimbali ya CCM katika Musoma, akianza na uzinduzi wa Shina namba tano Tawi la Veta Kata ya Mwisenge Veta, pia atakagua miradi ya maendeleo, na baadaye kufanya mkutano wa hadhara Musoma Mjini.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button