Kihongosi: Maamuzi ya vikao yaheshimiwe

TARIME: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi amesema msingi wa chama chao ni vikao, hivyo maamuzi yanayotolea katika vikao yanapaswa kuheshiwa.

Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 15,2026 alipotembelea na kuhudhuria Shina namba tatu Tawi la Buhemba Kata ya Bomani Jombo la Tarime Mjini ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa Mara.

Kihongosi alisema watu wanapaswa kuheshimu maamuzi ya vikao kwa sababu ndipo watu wanapokaa kufanya mipango na kukubaliana hivyo maamuzi ya vikao ndiyo maamuzi ya chama.

“Kiongozi aliyeiva itikadi ya CCM maamuzi ya mwisho ya vikao ndiyo maamuzi ya chama na wanachama hao, vyama vyetu au chama chetu tunasema msingi wa chama ni vikao, kwenye vikao tunakaa, tunapanga tunakubaliana tunasonga mbele,” amesema Kihongosi.

Kihongosi ameongeza kuwa kazi ya chama itafanywa na wanachama watiifu na wazalendo wa chama, hivyo ukiona kuna mtu ana mambo yake mengine huyo si mwanachama aliyoiva itikadi ya CCM.

Katika hatua nyingine amewataka zetu viongozi wa CCM walinde chama kwa sababu chama ndicho kimewapa heshima ya uongozi, hivyo waachane na mambo ambayo yanaharibu chama hiyo kwahiyo lazima tu maslahi yetu mapana yawe ndani ya chama.

“Jambo ninalopenda kulisisitiza hapa katika mkutano wetu huu wa ndani wana CCM tukipende chama kuliko kupenda watu ndani ya chama, maana yake chama kwanza watu baadaye,” amesisitiza Kihongosi.

“Ninacho maanisha hapa Tarime tunahitaji, umoja upendo na mahikamano ili kuwa na CCM imara na madhubuti lazima kama kuna makundi yafe, kama kuna mambo hayaeleweki yamalizwe ili Tarime Chama Cha Mapinduzi kiwe Imara”.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button