Wahitimu Taasisi ya Uongozi wahimizwa ubunifu

DAR ES SALAAM :WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewataka wahitimu Taasisi ya Uongozi kuwa waadilifu, wabunifu na uthubuti katika kazi na wenye tija kwa taifa.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam kwenye mahafali ya 9 ya taasisi hiyo na kusema kuwa mafunzo waliyopewa wakayafanyie kazi kwani uongozi sio cheo ni dhamana hivyo wakawatumikie vyema huko kazini.
Aidha, Ridhiwani amesema mafunzo waliyopata yakalete mageuzi na maendeleo endelevu kwani wamebadilika ukilinganisha na kipindi Cha awali kabla hawajapata mafunzo hayo na wawe wazalendo kwa taifa.
Naye, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Kadaru Singo amesema ni mahafali ya 9 wanaamini uongozi ni muhimu kufikia maendeleo hivyo programu hiyo inawajenga kukabiliana na madhaifu yao katika uongozi.



