CCM yasisitiza hakuna mkubwa kuliko chama

MARA: CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka wanachama wake kuvuja makundi, kwani chama hicho hakihitaji makundi bali umoja, upendo na mahikamano na hakitovumilia kuchukua hatua kwa yeyote atakayekiuka misingi na taratibu cha chama kwani hakuna mkubwa kulicho chama hicho.
Kihongosi ameeleza hayo leo Mei 16,2026 alipotembelea shina namba Tawi la Nyasaricho Kata ya Binagi Wilaya ya Tarime mkoani Mara, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika mkoa huo.

“Jambo ninaloomba kusisitiza hapa kama kuna makundi tuvunje makundi chama cha Mapinduzi hakihitaji makundi kinahitaji mambo matatu umoja upendo na mshikamano na tunaeema umoja ni ushindi,” amesema Kihongosi.
Ameongeza: “Sasa rai yangu uongozi wa chama ngazi ya Mkoa, Wilaaya Kata, Ngazi ya Tawi ngazi ya shina ambaye atabeba mtu kuliko kukibeba chama, endapo tutabaini hayo chama kitachukua hatua mata moja bila kuangakia umaarufu wako, uzoefu wala uwanachama wako matharani unakigawa chawa lazima hatua tuzichukue”.

Alisisitiza hakuna aliyemkubwa kuliko CCM kwani ni chama kikubwa na kimedumu kwa miaka mingi kwa sababu ina taratibu zake za kushughulikia mambo yake, kuna kanuni, katiba na miongozo ya chama ambayo kama kuna makosa yanafanyika kila kitu kipo wazi namna ya kuchukuliana hatua.
“Sitarajii kuona ndani ya Wilaya hii kuna makundi au kuna muendelezo wa Makundi au yaoo makundi na katika hili tutakuwa wakali kweli kweli kama ambavyo mwalimu Nyerere akituachia chama hiki chenye upendo lazima na sisi tuwakabidhi kizazi kinachokuja chama chenye upendo na kisichogawanyika,” amesisitiza Kihongosi.

Ameongeza kwa kumtaka Mwenyekiti wa CCM Wilaya kufanya kazi ikiwa kuna suala la makundi ili waweze kuwa wanachama wenye umoja upendo na amani katika Wilaya hiyo.
Akisoma ajenda ya kikao cha shina hilo Katibu wa Shina, Robert Werema amesema shina hilo lina jumla ya wanachama 150 hai waliosajiliwa kwenye mfumo wa kielektroniki na kupew akadi ni watu 120 na 30 bado hawajaingizwa kwenye mfumo.
Ameongeza kuwa waliondikishwa kwenye daftari ni watu 200 huku wengine wameshatangulia mbele za haki amewataka wanachama waendelee kusajiliwa ili waweze kupata kadi kwa mfimo wa kielektroniki.



