Washukuru uwepo wa wataalamu wa sheria

SHINYANGA: WAKAZI wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa Almas uliopo Mwadui Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameshukuru kuja kwa wataalamu wa msaada wa kisheria wa awamu ya pili ya Mama Samia Legal Aid .

Shukrani hizo zilitolewa na Diwani wa Kata ya Songwa, Abdul Ngolomore alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kutoa msaada wa kisheria kwa migogoro mbalimbali ikiwemo ardhi, mirathi, ndoa na matunzo ya watoto.

Ngolomore amesema mgogoro wa ardhi wa vijiji kuhusu mipaka kuingiliwa na mwekezaji kilio hicho kilianza tangu mwaka 2002 hivyo kuja kwa wataalamu wa msaada wa kisheria wataweza kusaidia kumaliza mgogoro uliopo.

Juma Kapina na George Magashi wakazi wa Idukilo wameeleza changamoto iliyopo wameshindwa kulima sababu ya migogoro ya mipaka ya vijiji na leo hii wamefika na kusikia kilio chao wanamatumaini makubwa haki itapatikana.

Ofisa mipango miji kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Barnaba Kapaya amesema tayari vijiji 38 kati ya 117 vimepimwa na kuwekewa mipaka na kuchorwa ramani.

Mkurugenzi kutoka Wizara ya Sheria na Katiba, Obson Paris amesema amefurahi wananchi kutoa kero hiyo sababu wamekuja kwaajili ya kutoa msaada wa kisheria wataondoka na vielelezo vyote nakuviwasilisha kwenye ngazi ya wilaya,mkoa na wizara husika na baadaye watawaletea majibu yaliyo sahihi .

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button