Kihongosi aweka mawe ya msingi ofisi za CCM Bunda

BUNDA: KATIBU wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi ameweka Jiwe la Msingi katika Jengo la Kitega uchumi na Ofisi ya CCM Tawi la Kibara B Kata ya Kibara Jimbo la Mwibara ambayo imegharimu kiasi cha Sh milioni 147 katika utekelezaji wake.

Pia Kihongosi amewekajiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Kata ya Nyamakokoto Jimbo la Bunda ambayo utekelezaji wake unatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh milioni 30.

Kihongosi ameweka Mawe ya Msingi katika ofisi hizo leo Mei 17,2026 alipofika katika Wilaya ya Bunda ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Mkoa wa Mara.

Mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Tawi ya Kibara B Kihongosi aliwapongeza wanachama na wadau waliyoshiriki katika mradi huo, akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama kwa kusimama kufanikisha hilo.

“Chama ngazi ya taifa tumefarijika na mradi huu lakini tunampongeza ndugu yetu Wilson Mukama kwani niwana chama wachache ambao wanaweza kuchangia miradi ya chama chao.”amesema Kihongosi.

Kihongosi ameongeza kwa kuwataka wana CCM kuendelea kukarabati miundombinu ya chama na kuendelea kukipigania chama, kulinda miundombinu pamoja na kulinda amani, umoja na mshikamano wa nchi.

Akisoma taarifa ya Mradi huo Katibu wa CCM kata ya Kibara, Charles Adam amesema mradi huo hadi sasa umefikia asilimia 87 ya utekelezaji na wapi katika hatua za mwisho za utekelezaji, wanatarajia kuendelea na ufungaji wa madirisha ya vioo, kuweka vigae, umeme na vinginevyo.

Pia hadi sasa jumla ya fedha 147.56 zimetumika hadi ulipofikia na unatarajiwa kukamilika mwaka huu.

Katika hatua nyingine Kihongosi ameweka jiwe la Msingi katika jengo la ofisi ya Kata ya Nyamakokoto ambayo inatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh milioni 30 katika utekelezaji wake.

Pia ilielezwa kuwa hadi sasa mradi huo umefikia asilimia 80 ya utekelezaji wake na wapo kwenye hatua ya ukamilishaji wa boma, upauaji, kuweka madirisha kufunga vifaa vya umeme na kuweka umeme.

Pia wakati huo huo ametembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM Wilaya ya Bunda inayojengwa katika Kara ya Kabarimi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button