RC Mwanza aagiza Sh milioni 111 ilipwe fidia wakazi Mwanza

MWANZA: MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda ameiagiza Halmashauri ya jiji la Mwanza kulipa fidia ya ardhi ya thamani Sh milioni 111 kwa wakazi 26 wa mitaa wa Luchelele Ziwani,Kisoko na Kasamiko iliopo katika kata ya Luchelele.
Deni hilo limetokana kupitia mradi wa kupanga,kupima na kumilikisha viwanja katika kata ya Luchelele mwaka 2006.
Mtanda ametoa rai hiyo leo wakati wa mkutano wa hadhara katika mtaa wa Nganza. Mtanda alisema watu hao 26 wanatakiwa kulipia fidia yao ndani ya miezi mitatu kuanzia mwezi huu Mei.
“Halmashauri ingeanza kuwalipa madeni madogo madogo ya fidia kwa wakazi wa Luchelele. Kisha wanaanza kuwalipia yena fidia wakazi wengine wenye madeni makubwa” alisema.
Mtanda amesema katika kata ya Luchelele kuna maeneo ya wazi ya viwanja 76 yametengwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza pia maeneo haya ni kwaajili ya maeneo ya Umma.
“Maeneo ya wazi yasiokuwa na matumizi yanatakiwa kurudishwa kwa wananchi wenyr maeneo yao ili kupunguza mzigo wa kulipa fidia kwa wananchi haswa maeneo ya mtaa wa Kisoko na Kasamiko” alisema.
Vile vile, Mtanda ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Wilaya ya Ilemela kwa kuweza kuanza kulipa madeni ya fidia ya wakazi wa kata ya Sangabuye ambapo mpaka sasa fidia iliyolipwa mpaka sasa ni Sh milioni 200.



