Wahandisi 1,000 kushiriki kongamano uhandisi

DAR ES SAAM: ZAIDI ya wadau 1,000 wanatarajia kushiriki Kongamano la 12 la wahandisi lenye lengo la kubadilishana uzoefu katika taaluma zao ambalo litafanyika tarehe 13 hadi 17 mwezi Septemba jijini Dar es Salaam.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam, Mhandisi Asa Mwaipopo Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET) wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kongamano hilo litahudhuriwa litafunguliwa na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi.

“Kongamano hili linafanyika kila mwaka mwaka katika nchi mojawapo ya Afrika mwaka huu Tanzania umepata fursa kuwa mwenyeji na Taasisi ya Wahandisi Tanzania imechagua kufanya hapa Dar es Salaam ,Tanzania ni mwana Chama wa Shirikisho la Uhandisi FAEO na pia wa Shirikisho la Vyama vga Ubanisi Duniani WFEO kupitia ushirikiano huo Taasisi inafanya kazi kwa pamoja na UNESCO katika kukuza na kuhamasisha Sekta ya uhandisi barani Afrika na Duniani kote,”amesema Mwaipopo.

Kwa Upande wake, Mhandisi Martin David Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano hilo amesema kwenye kongamano hilo watajadili matumizi ya Akili Unde kwani Dunia ya sasa inabadilika hawana budi kubadilika nayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button