Wanawake 26,000 wajitokeza msaada wa kisheria Ushetu

SHINYANGA: WANAWAKE zaidi ya 26,000 wamejitokeza kwenye kampeni ya awamu ya pili ya msaada wa kisheria kati ya wananchi 46,400 waliojitokeza kwa kipindi cha siku 15 kilichofanyika kutoa elimu na kutatua migogoro mbalimbali katika halmashauri ya Ushetu. wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mratibu wa kampeni hiyo Halmashauri ya Ushetu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Daniel Mbaki amesema hayo wakati wa kufunga kampeni hiyo huku akieleza wamevifikia vijiji 69 kwenye kata 20 zilizopo halmashauri hiyo.

Mbaki amesema kupitia kampeni ya msaada wa kisheria wanawake wameongoza kujitokeza zaidi ukilinganisha na idadi ya wanaume ambapo migogoro 101 ilibainika kwa masuala ya ardhi,mirathi na matunzo ya watoto.

“Migogoro 101 iliyopatikana kati ya hiyo migogoro 33 imetatuliwa na migogoro 60 imeendelea kufanyiwa kazi kwa na kupatiwa ufumbuzi na changamoto kubwa iliyopo ni baadhi ya wananchi kuwa na imani za kishirikina kwa kuogopa kuripoti migogoro,”amesema Mbaki.

Mbaki amesema uandikaji wa wosia bado changamoto hivyo alitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate sheria ili waweze kupata haki.

Mbeki amesema kampeni hii wizara ya katiba na sheria imejitokeza kusimamia na hata wananchi watakapo kuwa wanafanya kitu chochote hasa mauziano ya nyumba ,shamba na viwanja waandikishane kwa mkataba ili kuepusha migogoro.u

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button