Maarifa yahitajika kuendeleza sekta ya madini

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde amewataka wanafunzi kutumia maarifa, ujuzi na uzoefu ambapo ukitumika ipasavyo unaweza kuifanya Tanzania ipige hatua kubwa zaidi ya maendeleo kupitia rasilimali zake za madini.

Hayo ameyasema leo Juni 9, akiwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) wakati akifungua maonesho ya 11 ya wiki ya Tafiti na Ubunifu na kusema kuwa maadhimisho hayo yatasaidia kuibua watafiti na wabunifu jambo litakalosaidia nchi kuwa na watu wenye tija na maendeleo.

“Nchi yetu ya Tanzania ina eneo la takribani kilomita za mraba 945,000 katika eneo hilo tumefanikiwa kufanya Geological Mapping kwa asilimia 97,Aeromagnetic Survey kwa asilimia 100 na tafiti nyingine muhimu za awali.

“Hata hivyo changamoto kubwa iliyopo ni kwamba utafiti wa kina unaweza kubaini maeneo yenye uwezekano mkubwa wa Madini(Anomalies na magnetic Targets)umefanyika katika takribani asilimia 16 Tu eneo lote la Tanzania,” amesema Mavunde.

Kwa Upande wake, Prof William Anangisye, Makamu Mkuu wa UDSM amesema maonesho hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika taifa yamechangia kutangaza watafiti ,wabunifu na wasomi hivyo kuvutia ushiriki katika miradi mikubwa ya kimkakati ya kitaifa na kimataifa kutokana na ubora wa kazi zao.

Naye, Prof. Nelson Boniface, Naibu Makamu Mkuu Wa Chuo Utafiti UDSM amesema kazi 338 zilizowasilishwa katika ngazi za idara kazi 210 zimechaguliwa katika maonesho hayo kati ya kazi hizo asilimia 66 ni kazi za wanafunzi huku asilimia 66 ni za wafanyakazi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button