“Tafiti za NIMR ziwe suluhisho changamoto za afya”

ARUSHA: Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa ameiagiza Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa (NIMR) kuendelea kuzalisha tafiti na ubunifu zinazosaidia kutatua changamoto mbalimbali za afya nchini

Mchengerwa ameyasema hayo leo jijini Arusha katika ufunguzi wa Kongamano Kuu la Mwaka la Kisayansi la 33 liloloanza leo hadi Juni11.

Amesema moja ya changamoto kubwa inayokwamisha manufaa ya tafiti kuwafikia wananchi kwa haraka ni kuchelewa kwa maamuzi kutoka kwa mamlaka husika huku akiongeza kwa Tanzania ina watafiti wenye uwezo mkubwa ambao wamekuwa wakitoa majibu ya kisayansi kwa changamoto nyingi zinazoikabili nchi.

“Mara nyingi watafiti hukamilisha kazi yao kwa kutoa ushahidi na mapendekezo, lakini utekelezaji wake hukwama kutokana na baadhi ya viongozi au taasisi kusita kufanya maamuzi muhimu,” amesema.

Amesisitiza kuwa taifa haliwezi kunufaika kikamilifu na tafiti ikiwa matokeo yake yataendelea kubaki kwenye ripoti na makabrasha badala ya kutafsiriwa kuwa hatua za vitendo kwani tafiti nyingi zinazofanywa na NIMR zimepata kutambuliwa kimataifa na kutumiwa na nchi nyingine katika kuandaa sera, sheria na mikakati ya afya

“Hii inaonesha kuwa Tanzania ina hazina kubwa ya maarifa ambayo inaweza kutumika kuimarisha afya ya wananchi na kuchochea maendeleo ya taifa na tunao watafiti wengi wenye uwezo wa kutafuta suluhisho”

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button