Tantrade yatangaza mambo mazuri maonesho ya Sabasaba

DAR ES SAlAAM :Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo Ya Biashara (TanTrade Dk,Latifa Khamis amesema maonesho ya 50 ya Sabasaba ya mwaka kwa waoneshaji wa ndani ni 3,752 ukilinganisha na mwaka Jana 3,670 huku kukiwa na nchi 23 na matarajio zitaongezeka nyingine.

Akizungumza leo, mkurugenzi huyo amesema maonesho yataanza Juni 28 hadi Julai 13, 2026 na yatafanyika sambamba na maadhimisho ya Jubilee ya Dhahabu (Golden Jubilee,) ambapo kutakuwa na matembezi maalumu ya uzinduzi Juni 27, 2026 viwanja vya farasi yakiongozwa na Spika wa Bunge Mussa Azzan .

“Maonesho ya Mwaka huu yatajumuisha programu mbalimbali ikiwemo siku maalumu ya taasisi mbalimbali, mikutano ya biashara na uwekezaji pamoja na majukwaa ya kuwaunganisha wafanyabiashara wa ndani na nje.

“Moja ya vivutio vikubwa vy mwaka huu ni usiku wa Jubilee ya Dhahabu utakaofanyika Julai 6, 2026 katika hafla hiyo kutakuwa na maonesho ya nyaraka za kihistoria,” amesema Latifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button