Waziri wa Fedha atoa maagizo TRA

DAR ES SALAAM: Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar ameielekeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha inaongeza makusanyo ya kodi ili kuendana na hali ya ukuaji wa uchumi unaoendelea kushuhudiwa nchini.

Waziri wa Fedha ametoa maagizo hayo akiwa katika banda la TRA ndani ya Maonyesho ya Biashara ya 50 ya Kimataifa (Sabasaba) na kusisitiza kuwa TRA inapaswa kuonyesha ongezeko la makusanyo ya kodi ili kuakisi kiwango cha ukuaji wa uchumi.

“Serikali imeedelea kutekeleza mipango inayoimarisha hali ya uchumi na hivyo TRA inapaswa kuongeza ubunifu katika makusanyo ya kodi ili kuendana na hali ya ukuaji wa uchumi hivi sasa,” alisema Balozi Omar.

Aidha, amepongeza ushirikishwaji wa vilabu vya kodi ndani ya maonyesho na kuwaasa wanafunzi wa vilabu hivyo kuhakikisha wanafikisha elimu ya kodi kwa jamii ikiwemo kuhamasisha jamii kutokukwepa kodi kwa maendeleo ya nchi.




F8BET thương hiệu giải trí cùng worl cup 2026