Barabara kuchochea ukuaji uchumi Longido

ARUSHA: KUKAMILIKA kwa ujenzi wa Barabara ya Samia Longido Girls kunatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi wa Wilaya ya Longido kwa kuboresha usafiri, mawasiliano, biashara na fursa za uwekezaji

Kauli hiyo ilitolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, wakati wa ukaguzi na uwekaji wa jiwe la msingi wa mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 0.84.

Amesema barabara hiyo itarahisisha usafiri wa wananchi, kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii na kufungua fursa mpya za shughuli za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Longido, Mhandisi Lawrence Msemo, amesema barabara hiyo ina urefu wa jumla wa kilometa 0.84, ambapo awamu ya kwanza yenye urefu wa kilometa 0.3 katika Kijiji cha Oltepesi, Kata ya Orbomba, imegharimu Sh milioni 395.

Ameeleza kuwa mradi huo ulianzishwa kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Longido Girls, huku kazi zilizobaki zikihusisha ujenzi wa mifereji ya maji.

Kwa mujibu wa Msemo, barabara hiyo inaunganisha Mji wa Longido na Shule ya Sekondari ya Wasichana Longido Girls, ambayo ni shule muhimu ya Mkoa wa Arusha, hivyo itarahisisha usafiri kwa wanafunzi, walimu na wananchi wa maeneo jirani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button