Wasio na uwezo kupima afya bure afya Arusha

ARUSHA: WAZIRI wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Paul Makonda amesema watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha katika Jiji la Arusha watapata huduma ya kupima afya bure kila mwaka sambamba na huduma ya matibabu.

Makonda amesema hayo leo Julai 14 katika kambi ya matibabu Uwanja wa Shekh Amri Abeid na kuratibiwa na ofisi yake.
Amesema mara nyingi utaratibu wa kupima afya hufanywa na watu wenye uwezo wa kifedha lakini hilo litakuwa tofauti kwa wakazi wa jiji hilo.

Makonda amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa madaktari wake bure na hospitali za umma kwenda Jijini Arusha kutoa huduma ya matibabu bure hivyo wananchi wa Jiji la Arusha wanapaswa kuitumia fursa hiyo kikamilifu katika maisha yao ya baadaye.
‘’Madaktari wote bingwa nchini wameitikia wito wa kupiga kambi ya matibabu hapa Arusha hivyo basi nataka kuona kila mkazi wa Jiji la Arusha mwenye changamoto ya afya afike kupata tiba bila malipo,” amesema Makonda.

Aidha, aliwataka wakazi wa Arusha kuwa na tabia ya kupima afya mara moja kwa mwaka na kuacha mara moja tabia ya kunywa dawa za hospital bila kupata idhini ya daktari kwani kwa kufanya hivyo ni kutaka kujiletea matizo yasiyokuwa na msingi.
Waziri Makonda pia aliwashukuru wale wote walioshiriki kufanikisha hilo ikiwa ni pamoja na wale waliotoa msaada wa vifaa tiba na madawa kwa ajili ya wakazi wa Jiji la Arusha kusema kuwa wamefanya jambo muhimu sana kwa Mungu na wakazi wa Arusha.

Alisema hadi jana zaidi ya wakazi 6,500 wa Jiji la Arusha na nje ya Jiji wamejiandikisha kupata huduma ya matibabu katika kambi hiyo ya siku saba na wamefanikiwa kupata huduma ya tiba na kupimwa afya.
Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kambi hiyo ya tiba, Dk Charles Mkombachepa amesema kuwa mwitikio wa watu ni mkubwa sana na huduma kwa madaktari wa magonjwa yote makubwa na madogo wanaifanya kazi hiyo kwa weledi bila changamoto yoyote.




F8BET thương hiệu giải trí cùng worl cup 2026