Wafanyabiashara wapya wasogezwa mfumo rasmi

DAR ES SALAAM: WAFANYABIASHARA wapya wametakiwa kusajili namba za utambulisho wa mlipakodi (TIN) ili kunufaika na msamaha wa kodi kwa mwaka mzima, kama ilivyoelekezwa na Serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda ametoa wito huo akiwa ziarani katika mikoa ya Kikodi Temeke na Ilala kwenye Kituo cha Kodi cha Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.

Amesema utaratibu huo utasaidia kukuza biashara, kuongeza idadi ya walipakodi na kuwezesha biashara nchini huku akiwataka Walipakodi kuendelea kukitumia kitengo cha kuwezesha biashara ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

“Dawati la kuwezesha biashara kwenye kila mkoa na vituo vyetu vya kodi zinaendelea kutoa huduma za kuwezesha biashara kwa kutatua changamoto, kutoa ushauri na kuwaunganisha walipakodi na vyombo vya fedha hivyo endeleeni kulitumia kikamilifu” amesema Mwenda.

Naye Kaimu Meneja mkoa wa Kodi Temeke Suleiman Mwadini amewashukuru Walipakodi kwa kuendelea kulipa kodi kwa uaminifu na kuwaita wafanyabiashara wapya kuchangamkia fursa ya msamaha wa kodi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button