Kigoma watakiwa kutumia fursa za biashara

KIGOMA’ Mkuu wa mkoa Kigoma Balozi Simon Siro, amewataka wafanyabiashara wa mkoa huo kutumia fursa ya mkoa huo kupakana na nchi za ukanda wa maziwa makuu kufanya biashara zao kuwa na tija kubwa wakati huu ambao serikali imeweka mazingira mazuri kwao.

Balozi Siro alisema hayo katika kikao kilichoandaliwa na Chemba ya Taifa ya Biashara (TNCC) na wafanyabiashara wa Mkoa Kigoma, ili kutoa taarifa ya mabadiliko ya muundo na wajibu wa sasa wa TNCC kutoka iliyokuwa Chemba ya wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).

Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya Kigoma, Dk Rashid Chuachua, mkuu huyo wa mkoa alisema wakati huu ambao mkoa huo umeteuliwa kuwa wa biashara na uchumi kwa ajiili ya soko la nchi za ukanda wa maziwa makuu, serikali imefanya mambo mengi kuchochea shughuli za biashara.

Alisema katika kutekeleza hilo serikali imeweka mazingira rahisi na wezeshi ya uwekezaji na ufanyaji wa biashara wenye tija, hivyo wafanyabiashara wa Kigoma wanapaswa kutumia nafasi hiyo kutekeleza wajibu wao, baada ya serikali kufanya majukumu yake.

Awali akitoa maelezo kuhusu mkutano huo unaojulikana kama Kigoma Bussines Breakfast, Meneja wa TNCC Mkoa Kigoma, Prosper Guga alisema kuwa baada ya mabadiliko ya muundo na majukumu ya TNCC, hawajapata nafasi ya taasisi hiyo na wafanyabiashara kukaa pamoja kuelezana kuhusu mabadiliko hayo, ili waweze kuuliza na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusiana na taasisi hiyo.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button