Watanzania watakiwa kuchangamkia fursa zabuni AFCON

DAR ES SALAAM; Kampuni, taasisi, watoa huduma wenye uwezo na sifa stahiki wa Tanzania wamehimizwa kuchangamkia fursa mbalimbali za zabuni zilizotangazwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuelekea maandalizi na uendeshaji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON2027).

Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa Kamati ya Ndani (LOC),  Neema Msitha, amesema CAF imetangaza fursa mbalimbali za zabuni zinazohusiana na maandalizi na uendeshaji wa mashindano yake, ikiwamo AFCON 2027, ambayo Tanzania itaandaa kwa kushirikiana na Kenya na Uganda.

“LOC inawahimiza Watanzania wenye uwezo, sifa na nia ya kushiriki fursa hizi kufuatilia matangazo rasmi ya zabuni hizo kupitia tovuti ya CAF, ili kusoma masharti ya kila zabuni na kuwasilisha maombi yao kufuatana na taratibu na muda uliowekwa na shirikisho hilo,” amesisitiza Msitha.

Amesema fursa hizo zinahusisha maeneo mbalimbali, yakiwamo michezo, biashara, huduma za kitaalamu, teknolojia, masoko, usafirishaji na malazi, pamoja na huduma nyingine zitakazohitajika kulingana na matakwa ya kila zabuni.

“Tunawajulisha Watanzania, taasisi, kampuni na wadau wenye uwezo na sifa stahiki kuwa CAF imetangaza fursa mbalimbali za zabuni zinazohusiana na maandalizi na uendeshaji wa mashindano yake, ikiwamo AFCON 2027,” amesema Msitha.

Kwa mujibu wa Msitha, fursa hizo ni muhimu kwa kampuni na watoa huduma wa ndani kupata nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na maandalizi na uendeshaji wa AFCON 2027.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ https://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button