‘Kisa cha Mpemba’ kilitokea Tabata

MSANII wa muziki wa dansi kutoka Twanga Pepeta, Luizer Nyoni maarufu kama Luizer Mbutu amesema wimbo maarufu wa Kisa cha Mpemba ulitokana na tukio halisi lililotokea Tabata, Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar-es-salaam katika mahojiano maalum na  Daily news Digital Luizer amesema kisa hicho kilimhusu Mpemba, aliyekuwa akihudumia familia ya mtu mwingine kwa uaminifu kabla ya mambo kubadilika na kuingia katika uhusiano usiofaa na mke wa mwenye nyumba.

“Wimbo wa Kisa cha Mpemba ni maisha halisi. Wahusika walikuwepo na matukio yaliyosimuliwa ndani ya wimbo yalitokea,” amesema. SOMA: Mambo yameiva tamasha la dansi Mbeya

Amesema nyimbo za dansi mara nyingi hutokana na matukio ya kweli katika jamii, zikilenga kuburudisha na wakati huo huo kutoa mafunzo kuhusu uaminifu, maadili na kuheshimu mipaka katika mahusiano. Luizer amesema wasanii wana wajibu wa kutumia kazi zao kuelimisha jamii kwa kugeuza matukio yanayotokea katika maisha ya kila siku kuwa nyimbo zenye ujumbe wa kujenga.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button