TBS yasisitiza upimaji bidhaa za ujenzi

DAR ES SaLAAM: SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewasihi wahandisi na watumiaji wa bidhaa na malighafi za ujenzi kutumia huduma ya upimaji wa hiari ili kujiridhisha na ubora wa bidhaa hizo kabla ya kuzitumia katika miradi ya ujenzi.
Yona Afrika kutoka TBS ametoa wito huo leo Septemba 25, 2026 wakati wa Maonesho ya Wahandisi yaliyofanyika Dar es Salaam. Ameleza kuwa ubora wa bidhaa na malighafi za ujenzi ni msingi muhimu wa kuhakikisha usalama, uimara na ustahimilivu wa majengo na miradi mbalimbali.
Amesema TBS inatoa huduma ya Upimaji wa Hiari (Type Testing – TT) inayowawezesha wazalishaji, waagizaji, wasambazaji na watumiaji kujiridhisha kuhusu ubora na utendaji wa bidhaa na malighafi mbalimbali kabla ya matumizi.
 
Kwa mujibu wa Yona, huduma hiyo inafanywa na wataalamu wenye weledi kwa kutumia maabara zenye vifaa na mitambo maalumu, huku vipimo vikizingatia viwango na taratibu zinazotambulika kitaifa na kimataifa.

Kupitia wataalamu wenye weledi na maabara zenye vifaa na mitambo maalumu, TBS hufanya vipimo kwa kuzingatia viwango na taratibu zinazotambulika kitaifa na kimataifa. Hii husaidia kutoa taarifa muhimu kuhusu sifa na utendaji wa bidhaa au malighafi zinazokusudiwa kutumika.

Usisubiri changamoto ijitokeze ndipo uchukue hatua. Kama wewe mtumiaji wa bidhaa na malighafi za ujenzi, fika TBS na tumia huduma ya Type Testing ili kujiridhisha kuhusu ubora kabla ya matumizi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button