Tanzania yashuka ubora viwango Fifa

DAR ES SALAAM; Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshuka kwa nafasi tatu kwenye chati ya viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), huku Rwanda ikipanda kwa nafasi tisa katika chati hiyo ya mwezi Oktoba, 2026.
Viwango vilivyotolewa mwanzoni mwa Septemba 2026, Tanzania ilikuwa ya 112, lakini ya viwango vilivyotolewa leo Oktoba 7, 2026 Tanzania ni ya 115, huku Rwanda ikiwa ya 119 ikipanda nafasi tisa.
Michezo ya karibuni Tanzania ‘Taifa Stars’ ilitoka sare ya bao 1-1 na Madagascar mchezo uliofanyika nchini Morocco Septemba 29, ambapo awali Septemba 25 ilifungwa nyumbani mabao 0-2 na Guinea Bissau Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar yote ikiwa ni michezo ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.
Kwa mujibu orodha hiyo Hispania imeendelea kushika nafasi ya kwanza duniani ikifuatiwa na Argentina, Ufaransa na England. Kwa Afrika Morocco ndiyo ipo kumi bora ikishika nafasi ya saba.



