‘Tunalenga ajira zaidi nchi za Ghuba’

DAR ES SALAAM; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu (kulia), akiwa pamoja na Waziri wa Kazi na Kinga ya Jamii wa Jamhuri ya Kenya, Alfred Mutua (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba, wakati wa Mkutano wa Pili wa Doha Dialogue, jijini Dar es Salaam.
Kwenye mkutano huo pamoja na mambo mengine ilielezwa kuwa Tanzania inatarajia kupata fursa zaidi za ajira katika nchi za Ghuba, zikiwemo nafasi za kitaalamu kwa madaktari, wauguzi, wafamasia na wahandisi.



