Mradi wa barabara Bulyanhulu kukamilika Disemba

SHINYANGA: MRADI wa ujenzi wa barabara ya Kahama Manzese hadi Kakola, katika Kata ya Bulyanhulu, yenye urefu wa kilomita 73, unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba mwaka 2026.
Hayo yamesemwa na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Marco Bee, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo la mradi huo, ulioanza rasmi kutekelezwa mwezi Juni mwaka 2024.
Mhandisi Bee amesema mradi huo umeleta mafanikio mbalimbali, ikiwamo kutoa ajira rasmi kwa watu 460, ambapo Watanzania ni 418 na raia wa China ni 42.

Amesema hadi sasa, sehemu ya barabara hiyo kutoka Kahama Manzese imekamilika kwa urefu wa kilomita 36, huku kukamilika kwa mradi mzima kukitarajiwa kuongeza shughuli za kiuchumi na kurahisisha usafirishaji.
Amesema pia taa zitawekwa katika maeneo yenye makazi ya watu, ikiwamo eneo la Segese ambalo lipo katikati ya barabara hiyo.
Kwa mujibu wa Bee, katika eneo hilo, kazi kubwa imekamilika na kinachobaki ni kuweka alama za barabarani pamoja na mapambo yanayohitajika.
Amesema pia kalvati za boksi 14 zimejengwa kwa asilimia 100, huku kalvati za mabomba 148 zikiwa zimejengwa, sambamba na kuinua matuta kwa kiwango cha juu ili kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na maji wakati wa mvua, hasa kipindi cha mvua za El Niño.
Naye Mhandisi Samson Mgina amesema kipande kinachoendelea kujengwa kwa sasa ni uwekaji wa tabaka la saruji, huku hatua hiyo ikielekea kukamilika kabla ya kuanza kuweka lami.
Amesema kutoka mwanzo wa mradi hadi eneo ambalo ujenzi wa tabaka la juu unaendelea, kazi imefikia kilomita 60, huku utekelezaji wa mradi mzima ukiwa umefikia asilimia 89.

Mgina amesema eneo la kuzalisha na kusaga mawe limegawanywa katika hatua nne ili kupata mawe na kokoto zenye viwango vinavyohitajika katika ujenzi wa barabara.
Amesema eneo hilo pia lina mtambo wa kusaga mawe na kuchanganya zege, hali inayosaidia kuongeza kasi ya utekelezaji wa kazi.
Mradi huo umefadhiliwa kwa fedha kutoka Kampuni ya Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kushirikiana na Serikali, huku mkandarasi akiwa ni China Construction Engineering Civil Company (CCECC).




VoyageNoka blog еst unn guide pour voyager գui vous aide à organiser սn voyage avec des voyage conseils simples, pratiquess et inspirants.
Ɗécouvrez ddes astuces terrain pour savoir commеnt
voyager аu Japon, préparer ᥙn road trip Italie, choisir ᥙne destination vacances été ⲟu encore mieux utiliser une sélection ԁe destinations.
Avec VoyageNoka, profiotez de recommandations honnêtеs sսr les budgets voyage afin ԁе voyager plus sereinement, éviter le stress et trouver l’inspiration ρоur
vօs prochaines aventures. Ԛue vouѕ souhaitiez préparer սn ⅼong
séjoսr, VoyageNoka centralise l’essentiel
рoսr vօus aider à voyager mieux, ⲣlus simplement еt avec plus de confiance.