Mechi zote mbili za Simba CAF kupigwa Uhuru

DAR ES SALAAM: Simba imetangaza rasmi ratiba ya michezo yake miwili dhidi ya FC 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), huku mechi zote zikitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Ratiba hiyo imetangazwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, leo ikieleza kuwa mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 20, 2026, huku wa marudiano ukipangwa Oktoba 25, mwaka huu.

Awali, mchezo wa kwanza ulipangwa kuchezwa nje ya Tanzania, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo), kabla ya ratiba kubadilika na michezo yote miwili kuhamishiwa Uwanja wa Uhuru.

Kwa Simba, michezo hiyo ni muhimu katika harakati za kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo ushindi wa jumla dhidi ya FC 15 de Agosto utaiwezesha kusonga mbele katika mashindano hayo.

Simba italazimika kutumia vizuri nafasi ya kucheza nyumbani katika michezo yote miwili ili kutimiza lengo hilo, huku ikihitaji kupata matokeo mazuri katika mikondo yote miwili ya pambano hilo.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Cash earning job to earns more than $700 per day. getting paid weekly more than $3500 or more simply doing easy work online. no special skills required for this job and regular earning from this are just awesome. all you need is 2 hrs a day for this job and earning are awesome. every person can get this by follow details here…

    THIS→→→→ http://Www.Payathome1.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button