Kihongosi awapa neno viongozi CCM

PWANI: KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewaonya watumishi wa umma wanaojiona wako juu ya chama hicho, akisisitiza kuwa hakitavumilia uzembe katika utekelezaji wa majukumu yao.

Kihongosi alisema CCM itaendelea kuwafuatilia watumishi wazembe na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa, bila kujali nafasi au hadhi ya mtu.

Akizungumza wakati akiwenga jiwe na msingi kwenye jengo la ofisi ya CCM kata ya Kimanzichana wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani, alisisitiza kuwa watumishi wa umma wanapaswa kutambua nafasi ya chama hicho katika kuunda serikali na kutekeleza sera na ilani ya uchaguzi ya chama hicho.

“Chama Cha Mapinduzi ndicho chama kilichounda serikali. Kwa hiyo, asitokee mtumishi yoyote wa umma akajiona yuko mkubwa kuliko chama,” alisema Kihongosi.

Alisema CCM ina wajibu wa kusimamia utendaji wa serikali ili kuhakikisha ahadi zilizotolewa kwa wananchi zinatekelezwa na rasilimali za umma zinatumika kuleta maendeleo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button