Viongozi Hanang’ watakiwa kushughulikia kero za wananchi

MANYARA; ‎Mkuu wa Wilaya ya Hanang’ mkoani Manyara, Vita Kawawa, amewataka viongozi na watendaji kuwasikiliza wananchi, kupokea maoni na kero zao, kuzitatua kwa wakati na kutoa mrejesho ili kujenga imani kwa Serikali.


‎
‎Kawawa ametoa agizo hilo leo wakati akifungua mafunzo ya uraia na utawala bora kwa viongozi na watendaji katika Wilaya ya Hanang’, amesisitiza kuwa viongozi wanapaswa kushughulikia malalamiko ya wananchi na kuhakikisha wanapata majibu na ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.
‎
‎Amesisitiza pia umuhimu wa kutoa kipaumbele kwa makundi yenye uhitaji maalumu, yakiwemo watu wenye ulemavu na wajane ili wapate huduma na haki stahiki bila ubaguzi.


‎
‎Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Prosper Kisinini, amewataka watendaji kuzingatia haki, utawala wa sheria na kutokuweka migogoro binafsi katika utekelezaji wa majukumu yao.
‎
‎Mafunzo hayo yamelenga kuwakumbusha viongozi wajibu wao katika kusimamia ustawi wa wananchi, kuimarisha demokrasia na utawala bora, pamoja na kuboresha utoaji wa huduma za Serikali.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button