Tanzania U-15 yaifunga Mauritius mashindano ya wavulana

BAKU:TIMU ya Taifa ya Tanzania ya wavulana chini ya umri wa miaka 15 imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mauritius katika michuano ya FIFA U-15 World Cup & Festival 2026 inayoendelea nchini Azerbaijan.

Mabao ya Tanzania katika mchezo huo uliochezwa leo yamefungwa na Yasir Jumbe, Shafi Kassim na Frank Hassan, ambao kila mmoja alifunga bao moja na kuiwezesha timu hiyo kupata ushindi.

Matokeo hayo yanaongeza uzoefu wa kikosi hicho katika mashindano hayo ya kimataifa yanayoshirikisha vijana kutoka mataifa mbalimbali, yakilenga kuwapa nafasi ya kuonesha vipaji vyao na kujifunza kupitia ushindani wa kimataifa.

Tanzania ni miongoni mwa timu zinazoshiriki mashindano hayo yanayofanyika jijini Baku, Azerbaijan, kuanzia Oktoba 24 hadi 30, 2026.

Katika mchezo wake wa awali, Tanzania ilipoteza kwa mabao 1-3 dhidi ya Zambia kabla ya kurejea na kuonesha uwezo wa kufunga mabao katika michezo iliyofuata, ikiwamo ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Montserrat.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button