Mabadiliko ya sheria PPP yavutia uwekezaji nchini

DAR ES SALAAM: MABADILIKO ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) yamefungua fursa kwa wawekezaji kushiriki katika miradi ya maendeleo nchini, huku yakiweka utaratibu wa migogoro ya uwekezaji kusikilizwa katika taasisi za kimataifa za utatuzi wa migogoro.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre), David Kafulila, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), akieleza kuwa mabadiliko hayo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini.

Kafulila amesema mwaka 2023 aliteuliwa na Rais kuwa Kamishna wa Ubia (PPP) chini ya Wizara ya Fedha, wakati huo ikiongozwa na Dkt. Mwigulu Nchemba, ambapo alipewa jukumu la kusimamia mabadiliko ya Sheria ya PPP.

Amesema miongoni mwa mabadiliko yaliyofanyika ni kuruhusu migogoro ya wawekezaji kusikilizwa katika taasisi za kimataifa za utatuzi wa migogoro ya uwekezaji, ikiwemo Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID).

Ameongeza kuwa hatua hiyo inaendana na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu kuimarisha mageuzi ya kisera, kisheria na kitaasisi yanayolenga kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini.

Kauli hiyo pia inaendana na wito wa Waziri wa Fedha, Balozi Omary Khamis, kuhusu umuhimu wa kufanya mageuzi ya jumla katika namna ya kufikiri, kupanga na kuendesha uchumi ili kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button