‘Fundisheni watoto sheria matumizi ya mitandao’

DAR ES SALAAM; Makamu Mkuu wa Chuo cha Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaaluma , Chuo cha Elimu ya Biashara Nchini (CBE), Profesa Robert Mashenene amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi ya shule za sekondari kuwafundisha wanafunzi hao sheria ya matumizi ya mitandao ya kijamii pindi wakiwa nyumbani.

“Wito wangu kwa wale wazazi wanaopenda kuwapa watoto wao simu za kisasa, ni jambo jema lakini mnatakiwa kuwajulisha ‘does and dots’ kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii,: amesema.

Mashenene ametoa wito wakati wa mahafali ya 26 ya kidato cha nne katika Shule za Green Acres Jijini Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Amesema wazazi wanatakiwa kukaa na watoto hao kuwafundisha namna ya kutumia simu hasa kupitia mfumo wa AI (Artificial intelligence) kwa manufaa ya taaluma zao.

Mashenene ameshauri pia wazazi kuwashirikisha watoto wao kufanya kazi za nyumbani ikiwemo kupika, kufua na kushiriki kufanya biashara za wazazi wao.

Mwalimu mkuu wa shule ya Green Acres Sekondari School Jonathan Kasabila amesema wazazi wanapaswa kuzuia na kudhibiti matumizi ya simu mara kwa mara kwa wanafunzi wakiwa nyumbani.

“Wazazi wanapaswa kuhakikisha watoto wao wanakuwa na muda maalumu wa matumizi ya simu, wawape semina watoto wao wajue ni nini wanapaswa kufanya kwenye simu na kwa muda gani,” amesema.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button