Wafanyabiashara Kahama wasisitizwa kuzingatia viwango

SHINYANGA; Wafanyabiashara wa vyakula na vipodozi katika Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga wametakiwa kuzingatia matakwa ya viwango,  ili kulinda afya ya watumiaji.

Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Wilaya ya Kahama, Glory Absalum, wakati akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Viwango Clinic inayoendeshwa na Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kwa Wilaya ya Kahama akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo DkFrancis Daud.

Amewasisitiza wafanyabiashara kuhakikisha wanasajili bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi, ikiwa ni pamoja na kuthibitisha ubora wa bidhaa zao kwa kumujibu wa sheria.

Kwa upande wake Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa Magharibi, Joseph Makene, amesema kliniki hiyo ni fursa kwa wananchi kukutana na wataalamu wa TBS kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na shirika hilo, kwani TBS imewasogezea huduma karibu.

Baadhi ya wafanyabiashara wakizungumza wamesema ni muhimu biashara zikafanyika kwa kuzingatia viwango ili kuepuka athari kwa mlaji na Mtumiaji.

Viwango Clinic inafanyika kati ya Novemba 16-20, 2026 , ambapo wafanyabiashara na wananchi willayani Kahama wanapata huduma mbalimbali ikiwemo uthibitishaji ubora wa bidhaa,usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi na elimu ya majukumu ya TBS  kwa wananchi na wadau mbalimbali.

Habari Zifananazo

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button