Kihongosi awabana wakandarasi makambako

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maji na umwagiliaji katika Halmashauri ya Mji wa Makambako, mkoani Njombe, kuhakikisha wanaikamilisha kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma hizo.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji unaohusisha ujenzi wa tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni mbili, wenye thamani ya Sh bilioni 23, pamoja na mradi wa umwagiliaji wenye thamani ya Sh bilioni 38. Kihongosi ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwa lengo la kuboresha huduma kwa wananchi.
Amesema wananchi hawana haja ya kuona majengo au miundombinu ya miradi isiyokamilika, bali wanatarajia kuona miradi hiyo ikikamilika na kuanza kutoa huduma zilizokusudiwa. SOMA: Kihongosi: Msiwasikilize wanaobeza maendeleo



