Kipindupindu chaua 31 Nigeria

WATU 31 wamefariki baada ya kuibuka wimbi jipya la kipindupindu nchini Nigeria Jumapili na Jumatatu katika vijiji 10 vya jimbo la Cross River, kusini mwa nchi hiyo.

Takwimu za Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Nigeria (NCDC), kimeeleza kuwa watu 1,569 walithibitishwa kukumbwa na ugonjwa wa kipindupindu kati ya mwezi Januari na Mei.

Wizara ya Rasilimali za Maji ya Nigeria ilisema jumla ya watu 3,598 waliaga dunia katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mwaka jana wa 2021.

Janga hilo la kipindupindu kuuwa watu katika hali ambayo, ni asilimia 14 tu ya wananchi wa nchi hiyo yenye idadi ya watu milioni 200 ndio wenye uwezo wa kupata maji safi na salama. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali za mwaka 2020.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button