Bashungwa: Mtwara hali ni shwari, pigeni kazi
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa amewahakikishia wananchi mkoani Mtwara kuwa hali ya usalama ni shwari, waendelee kufanya shughuli zao mbalimbali za kiuchumi.
Akizungumza leo mkoani Mtwara, waziri huyo amesema serikali inaendelea kudhibiti mianya yoyote ile ambayo inaweza ikajitokeza katika mipaka ya Tanzania.
Ameupongeza uongozi wa Mkoa Mtwara kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kuhakikisha hali ya usalama inaendelea kuwa shwari mkoani humo.
“Ziara yangu ni ya kawaida ya kuendelea kutembelea mipaka yetu na kuhakikisha ulinzi wa Watanzania pamoja na mali zao na mipaka ya nchi yetu inaendelea kuwa salama,” amesema Bashungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amesema kwa hali ni shwari na wananchi wanaendelea na shughuli zao mbalimbali za kuchumi katika meoneo yote mkoani humo.



