Yanga walia na ratiba Ligi Kuu
KOCHA Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, amesema changamoto kubwa inayowakabili kipindi hiki ni ratiba, kwani mechi zipo karibu karibu huku wachezaji wakikosa muda wa kutosha wa kupumzika.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha huyo ameeleza hali hiyo inasababisha wachezaji kucheza chini ya kiwango kutokana na uchovu waliokuwa nao, lakini pia kiufundi inamfanya kocha asimpe majukumu mengi mchezaji kutokana na uchovu.
“Sisi kama benchi la ufundi tunapambana kuwaandaa vizuri kwa lengo la kupata matokeo katika kila mchezo ingawa hawa ni binadamu nao wanatakiwa kupumzika kuna wengiine wapo kwenye mfungo,” amesema Kaze.
Yanga itacheza na Kagera Sugar kesho kwenye mchezo wa raundi ya 25 wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku miamba hiyo ya soka nchini ikijivunia rekodi nzuri ya kushinda mechi tatu zilizopita dhidi ya wapinzani hao kutoka Misenyi Bukoba.



