“Muda wa kubuni mbinu malezi duni”

SERIKALI imesema umefika wakati kwa kushirikiana na wadau kubuni mbinu na mikakati mbadala na za haraka kuja na afua za kisayansi zitakazowezesha kukabiliana na malezi duni ndani ya jamii.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Amoni Mpanju wakati akifungua Mkutano wa Taifa wa Wadau wa Malezi na kutokomeza ukatili dhidi ya watoto, Julai 13, 2023 Jijini Dodoma.

Mpanju amesema ukosefu wa elimu sahihi ya malezi na makuzi kwa wazazi na walezi hasa kwa watoto wa kiume ni miongoni mwa sababu zinazochochea mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa watoto na vijana nchini.

Mpanju amesema ipo haja kwa wazazi na walezi kuja na mfumo mzuri wa malezi wenye kushinikiza uwajibikaji wa baba na mama katika kuboresha malezi na ulinzi wa watoto.

“Kwa mujibu wa Taarifa ya Makosa ya Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji za Jeshi la Polisi kwa watoto kwenye kipindi cha Januari hadi Disemba, 2022 kulikuwa na matukio 12,163 (Wavulana 2,201 na Wasichana 9,962 nchini. Matukio yaliyoongoza ni Ubakaji (6,335), ulawiti (1,557) na Mimba za utotoni matukio (1,555).amesema Mpanju na kuongeza

“Serikali inathamini sana watoto kwa kutambua ndiyo rasilimali muhimu kwa ujenzi wa Taifa, hivyo imekuwa ikichukua hatua za makusudi kudhibiti vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kukuza maadili kwenye familia na jamii.” Amefafanua Mpanju.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button