Elimu kipaumbele rasilimali watu

WAZIRI wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema elimu ndio kipaumbele cha kwanza cha serikali katika kuzalisha rasilimali watu nchini.
Akitolea mfano wa matokeo chanya ya sera ya elimu bila ada iliyoanza kutumika 2016, na kupelekea mwamko mkubwa wa wananchi katika uandikishaji wanafunzi kujiunga na elimu ya awali, msingi na sekondari.
Ameyasema hayo leo Julai 25, 2023 katika Mkutano wa Kimataifa wa Wakuu wa nchi za Afrika kuhusu ‘Rasilimali Watu’ katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
“Kumekuwa na ongezeko la asilimia 38 ya uandikishaji wanafunzi wa elimu ya awali, na msingi na ongezeko la asilimia 44.6 ya ongezeko kwa elimu ya Sekondari.”
Aidha, Mwigulu amesema kwa sasa serikali imepiga hatua kwa kuondoa ada kwa elimu ya sekondari ya juu (Advanced Secondary Education Level) na malengo ya serikali ni kuondoa ada kufikia elimu ya vyuo vya kati.
Hata hivyo, Waziri huyo amesema kwa kuzingatia umuhimu wa rasilimali watu serikali inaendelea kuimarisha mfumo wa afya, uboreshaji na uenezaji wa mfumo wa TEHAMA nchi nzima na uinuaji wa sekta binafsi.
Itakumbukwa, Mkutano huo unafanyika kwa siku mbili mfulululizo, ambapo kesho Julai 26, 2023
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuungana na wakuu wa mataifa mbalimbali Afrika pamoja na viongozi wengine kushiriki mkutano na matarajio ni kuwa na Azimio la pamoja kama bara kuhusu rasilimali watu.
Mkutano huo unachagizwa kupitia mitandao ya kijamii na ‘hashtag’ #InvestInPeopl



