UN kuendelea kuwezesha vijana kwenye ubunifu

DAR ES SALAAM: KUELEKEA maadhimisho ya miaka 78 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini, shirika hilo limebainisha kuwa litaendelea kuchagiza matumizi ya teknolojia za kisasa katika kutanua wigo wa ajira kwa vijana na hivyo kuchagiza maendeleo endelevu
Akizungumza na wandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mratibu Mkazi wa UN Zlatan Millisic amesema shirika hilo limekuwa likishirikiana na taasisi na mashirika binafsi katika kuwawezesha vijana wabunifu kwenye sekta ya teknolojia ili kuwasaidia kujiajiri na kuboresha maisha yao.
Vilevile amesema kuwa wamejidhatiti kuwaongezea uelewa vijana hao ili kuwa na vigezo vinavyotakiwa katika kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha na hivyo kuongeza ushiriki wao katika maendeleo endelevu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sahara Ventures Mussa Kamata amesema wamejidhatiti kuboresha sekta za Ubunifu, Uwekezaji pamoja na Ujasiriamali kwa vijana ikiwa ni pamoja na kubadilisha mawazo ya kibunifu ya vijana kuwa tija iliyokusudiwa kwa ustawi wao na taifa kwa ujumla.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button