NM-AIST yaunga mkono mafunzo AI, sayansi data

ARUSHA: TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) imekabidhi vitendea kazi vya kompyuta 50 kwa wanafunzi 50 wa kambi maalumu ya Samia Scholarship katika Programu juu ya Sayansi ya Data, Akili Bandia (IA) na Sayansi Shirikishi.
Makabidhiano hayo ni kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (CoSTECH).

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo jijini Arusha, Makamu Mkuu wa Taasisi, Profesa Maulilio Kipanyula, amewapongeza wanafunzi kwa kujituma na kusisitiza dhamira ya serikali kupitia NM-AIST ya kuendelea kuwaandaa vijana kuchochea mageuzi ya kiteknolojia nchini.
Amesema tukio hilo ni sehemu ya mwendelezo wa juhudi za kuwawezesha wanufaika wa Samia Scholarship kupata maarifa ya kiwango cha kimataifa.

Naye, Dk Judith Leo ambaye ni Amidi wa Shule Kuu ya Sayansi ya Ukokotoaji na Uhandisi (CoCSE) amewahimiza wanafunzi kutumia vyema vifaa walivyopokea ili kuongeza ufanisi katika kujifunza na kufanya mazoezi ya vitendo.
Akizungumza baada ya kupokea kifaa chake, Sabrina Khamisi amesema kuwa kupokea vifaa hivyo vinatoa hamasa kubwa ya kujifunza kwa bidii zaidi kwani kwa sasa wanafunzi hao wataweza kufanya mazoezi ya vitendo na kujiandaa vizuri katika masomo ya akili bandia na sayansi ya data.

Huku mmoja kati ya waliopata kompyuta hizo, Elia Ricard amesema upataji wa kompyuta hizo ni fursa ya kipekee kwani vifaa hivyo vitamwezesha kufanya kuandika msimbo , uigaji katika teknolojia na miradi mingine ya kiteknolojia, na kuahidi kutumia kikamilifu rasilimali alizopata ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.
Programu hiyo mahsusi ilianza Septemba 15, 2025, ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa serikali wa kujenga wataalamu katika maeneo ya sayansi ya data, sayansi shirikishi na akili bandia ambapo dhamira hiyo imepewa uzito mkubwa na Rais wa Samia Suluhu Hassan wakati akifungua Bunge la 13 mnamo Novemba 14, 2025 Jijini Dodoma, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha elimu ya sayansi na hisabati.




I’m currently generating over $35,100 a month thanks to one small internet job, therefore I really like your work! I am aware that with a beginning cdx05 capital of $28,800, you are cdx02 presently making a sizeable quantity of money online.
Just Check ———>>>https://Www.Homeprofit1.site