Sagini afunguka ujenzi wa kituo cha polisi Butiama

MWANZA; Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini, ametoa ufafanuzi kuhusu kituo cha polisi kinachojengwa wilayani Butiama, mkoani Mara.

Ameeleza kuwa si kweli kwamba zaidi ya Sh millioni 800 zimeshatumika kwa ujenzi kama ilivyodaiwa kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni.

Kiasi hicho ni makadirio ya ujenzi, lakini mpaka sasa kiasi kilichokwishatumika ni Sh milioni 366 tu,” amesema leo Novemba 27, 2023 baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukafua miradi ya Jeshi la polisi Kanda ya ziwa.

“Na ni Sh millioni 500 tu zilizokwishatolewa kati ya makadirio yaliyofanywa. Hata hivyo, katibu mkuu wa wizara ameshaunda tume ya kuangalia kwa undani madai hayo, ili tupate ukweli zaidi.”

Ameongeza kwamba asilimia kubwa ya miradi hiyo, hasa ujenzi wa vituo vya polisi iko hatua nzuri, licha ya michache aliyokuta ikisuasua katika baadhi ya maeneo, ikiwemo mkoani Geita, akatoa maagizo ya kuongeza kasi ya kuikamilisha kwa wakati.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button