Serikali yafanya maboresho Kituo cha Afya Nyenge

SHILINGI milioni 800 zimetolewa na serikali  kuboresha huduma za afya kwenye  Kituo cha Afya Nyenge Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma.

Richard Marwa Ofisa muuguzi wa  kituo hicho,  akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo, amesema kuwa wananchi wa zaidi ya vijiji tisa vya Kata ya Nyenge na Kurugongo katika halmashauri ya Wilaya Kasulu wanatarajia kufaidika na maboresho hayo.

Marwa amesema kuwa awali kituo kilipokea Sh milioni 500 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya kituo hicho na baadaye kupokea Sh milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

Amesema kuwa fedha zimetumika katika ujenzi wa jengo jipya na kubwa la upasuaji, jengo la maabara, kliniki ya baba,mama na mtoto, chumba cha maiti na nyumba ya mtumishi ambapo utekelezaji wa majengo hayo umefikia asilimia 98.

Alieleza kwamba ujenzi wa majengo hayo unatokana na kuchakaa kwa majengo ya awali, lakini kuwepo kwa ongezeko kubwa la watu ambalo halikuwa likiendana na hali ya utoaji huduma kituoni hapo.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button