Super Nyamwela: Muziki wa asili unasoko ulaya kuliko bongo fleva

MKURUGENZI wa bendi ya muziki wa asili, Ubuntu Super Nyamwela ameweka wazi kwamba muziki wa asili unasoko kubwa nchi za Ulaya kuliko muziki wa Bongo Fleva.
Nyamwela anasema wasanii wa muziki wa asili wanamialiko mingi Ulaya kuliko wasanii wengine kwa sababu muziki wa asili unamashabiki wengi na unapendwa zaidi.
“Wasanii wa muziki wa asili na wasanii wa sarakasi ndiyo wanaongoza kufanya maonyesho nchi za Ulaya kuliko wasanii wengine ingawa muziki wa asili nchi za Afrika hawaupi thamani yake lakini nje wanauthamini mno,”amesema Nyamwela.
Nyamwela anawataka wasanii wa muziki wa asili kuutangaza muziki huo na kuongeza ubunifu ili uwe na mvuto katika soko la ndani.
“Hata kwenye mafanikio wasanii wa muziki wa asili wanamafanikio makubwa lakini hawapendi kujitangaza kama wafanyavyo wasanii wa bongo fleva,” ameeleza.



