Msanifu majengo Uingereza aalikwa Tanzania

BALOZI wa Tanzania nchini Uingereza amemualika msanifu nguli wa majengo nchini Uingereza, Sir David Adaje kufanya ziara nchini Tanzania kwa lengo la kufanya mhadhara kwa wabunifu wachanga.

Mwaliko huo ulitolewa katika mazungumzo kati ya Balozi Kairuki na msanifu huyo uliofanyika London na kuhudhuriwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Development Reimagined, Hannah Ryder ambapo Adaje alipokea mwaliko na kuahidi kufanya ziara hiyo wakati wowote ndani ndani ya mwaka huu.

Aidha katika mazungumzo hayo, msanifu huyo nguli wa majengo aliwaasa vijana wanaosomea utaalamu wa usanifu wa majengo (Architects) kubuni michoro ya kisasa inayoakisi utamaduni na mazingira ya kiafrika na kuacha kudurufu kazi za wasanifu wa mataifa mengine.

Pia, alionesha nia ya kuwasaidia vijana wa kiafrika wanaopenda kufanya kazi za usanifu kwa kuwajengea uwezo wa kufanya ubunifu wenye tija na maana kwa jamii zao.

Habari Zifananazo

Back to top button