Katibu ACT Wazalendo ziarani Pwani

DAR ES SALAAM; KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu, anatarajia kuanza ziara katika baadhi ya majimbo Chalinze na Kibaha Vijijini mkoani Pwani kuanzia Juni 14, 2024.
–
Kwa mujibu wa taarifa ya chama hicho, katika ziara hiyo, Ado atatembea kata kwa kata kuzungumza na viongozi na wanachama kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.



