Harris na Trump wakutana tena

MAREKANI : WAGOMBEA urais wa Marekani Kamala Harris na Donald Trump wamekutana tena katika Kumbukumbu ya Mashambulizi ya Septemba 11, muda mfupi baada ya wawili hao kushiriki mdahalo mkali uliofanyika hapo jana.
Harris na Trump walisimama pamoja mjini New Yok wakati wa kumbukumbu hiyo, na kisha kushikana mikono, ikiwa ni mara ya pili kuonana hadharani.
Rais wa Marekani Joe Biden alihudhuria kumbukumbu hiyo, ambayo ilihudhuriwa pia na mgombea mwenza wa Trump, J.D Vance. SOMA: Trump na Harris wachuana kwa karibu
Kabla ya kuhudhuria kumbukumbu hiyo ya Septemba 11, Trump alionesha kukasirishwa na utendaji wake kwenye mdahalo wa televisheni ambapo wataalamu wa siasa walidai kuwa Trump alishindwa na Kamala Harris.



