Wasanii tumieni mitandao kuhamasisha kujiandikisha

DAR ES SALAAM:MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke  Jomaary Satura amewahimiza wasanii wa Wilaya Temeke kutumia mitandao yao ya kijamii kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa 2024.

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo Ofisini kwake Jijini Dar es salaam alipokutana na wasanii hao ambapo kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura uchaguzi wa serikali za mitaa utaanza kesho mpaka tarehe 20 Oktoba huku uchaguzi wa serikali za mitaa ni Novemba 27.

Aidha Mkurugenzi huyo amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kujiandikisha, kugombea na kupiga kura ili waweze kupata kiongozi wanaomuhitaji na kuwaletea maendeleo yenye tija kwa jamii.

Satura amesema  kwenye  Halmashauri ya Temeke wameweka vituo zaidi ya 500 vya kujiandikishia  ili wananchi wasitembee umbali mrefu na waandikishaji wa vituo hivyo watalala leo kwenye vituo vyao vya kazi ili kurahisisha kazi kwa wananchi watakao wahi kesho kujiandikisha.

SOMA : Tamasha lahamasisha uchaguzi mitaa

Kwa upande wao wasanii Amani Temba na Deus Mihambo Wamesema watatumia mitandao ya kijamii kuwahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha.

 

Habari Zifananazo

Back to top button