Wazazi wakumbushwa kuwapeleka shule watoto

WAZAZI mkoani Mtwara wametakiwa kupelekea watoto shule ili waweze kupata elimu itakayowasaidia kukabiliana na fursa mbalimbali zinazojitokeza katika mkoa huo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji na kata ya Chawi iliyopo Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema watoto wasiyokuwa na elimu wataweza kuwa jamii inayolalamika.

Rai hiyo imetolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya mwanamke aishiye kijijini yaliyofanyika katika kijiji na kata hiyo ya chawi kwenye halmashauri hiyo ya mji Nanyamba mkoani humo.

‘’Selikali inawatambua na kuwajali wanawake wanaoishi vijijini na juhudi mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa kwa kuandaa mikakati ya kuwawezesha kielimu ili kuleta usawa wa kimaendeleo na amani nchini,’’amesema Sawala

Mwakilishi kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali la Baraza la Taifa (NACONGO) Baltazar Komba ametoa wito kwa maofisa wanaotoa mikopo kuzingatia vikundi vya wanawake wa vijijini hasa wale wenye miradi inayokabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wao baadhi ya wanawake kijijini hapo akiwemo Sharifa Mkuti ameelezea baadhi ya changamoto wanazokutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ushirikiano kutoka wanaume zao hasa suala la malezi ya watoto na kutoshirikishwa katika matumizi ya fedha zinazopatikana kupitia cha zao la korosho.

‘’Wanaume wengi wanamekuwa na hiyo tabia ukishazaa nao mwisho wa siku akishakutenga tu basi hakuna huduma zozote zile kwa watoto hata nini kwahiyo adhabu zote na huduma za watoto zinabaki kwa mama kwahiyo hiyo ndiyo hali halisi ya mazingira ya hawa wanaume wetu’’amesema Sharifa

Habari Zifananazo

Back to top button