Makachu kutangaza Zanzibar kimataifa

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema  Mchezo wa makachu  umekuwa fursa  nzuri ya kuitangaza Zanzibar kimataifa .

Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 24 Oktoba 2024 alipofika Bustani ya Forodhani Kuangalia Mchezo huo ambao umekuwa maarufu na kuvutia  wenyeji na wageni wengi wanaokuja nchini.

Aidha Rais Dk ,Mwinyi amewasisitiza Vijana wanaopiga makachu kuuendeleza Mchezo huo kwani umekuwa ukitizamwa na  kufuatiliwa na watu wengi sehemu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa upande wa Vijana wa makachu walitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dk, Mwinyi kwa kuonesha  mabango ya mafanikio ya Serikali katika  sekta  mbali mbali.

Tukio hilo ni muendelezo wa shamra shamra za  kupongeza mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya nane chini ya Uongozi wa Rais Dk.Mwinyi.

SOMA: Tangazeni fursa za uchumi Zanzibar

Habari Zifananazo

Back to top button