Sekta binafsi zivutwe kuwekeza nishati ya umeme

DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Vunjo (CCM), Dk. Charles Kimei amesisitiza umuhimu wa kuhamasisha uwekezaji kwa sekta binafsi katika uzalishaji wa nishati ya umeme nchini.

Akichangia taarifa ya mpango wa maendeleo wa taifa 2025/2026 bungeni Dodoma,Dk. Kimei amesema Mradi wa Uzalishaji wa Umeme wa Bwawa la Nyerere unaweza kuleta faida kubwa ya kiuchumi, kwa kuongeza mapato ya serikali na kuboresha huduma ya umeme nchini.

Dk. Kimei alitoa wito kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kushirikiana na wawekezaji wa sekta binafsi ili kuimarisha uzalishaji wa umeme.

Aliongeza kuwa, uwekezaji huu utasaidia kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na uhakika wa huduma ya umeme kwa muda mrefu, huku pia ukichangia katika maendeleo ya uchumi wa nchi.

SOMA: Uzalishaji umeme bwawa la Nyerere wakaribia

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button